16 Juni 2016 - 22:50
Georgia yazuia kutoa adhana nchini humo

Kiongozi wa ofisi ya Waislamu nchini humo amesema: viongozi wa serikali ya nchi hiyo wametoa maamuzi hayo kwa madai kwamba kutoa adhana kwa kutumia spika kunaleta adha kwa wananchi wake, hivyo wameamuru kutoa adhana hiyo ndani ya msikiti pekee

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mkuu wa idara ya Waislamu nchini humo akiashiria kuzuiliwa kwa kupazwa sauti ya adhana kwa kutumia spika katika misikiti ya nchi hiyo kwa madai kuwa inawaletea adha wananchi alisema: viongozi wa Georgia kwa madai walioyataja kuwa sauti ya adhana inaleta adha kwa wananchi wa nchi hiyo, hivyo kuwataka Waislamu kutopaza sauti ya adhana kwa kutumia spika na kutosheka kutoa adhana ndani ya msikiti yao pekee.
 Aidha aliongeza kusema kuwa: mimi napingana na maamuzi hayo kwani Wakristo hupiga kengee katika makanisa yao bila ya kuzuiliwa, hivyo haipaswi kuzuiliwa haki ya kutoa adhana kwa Waislamu nchini humo.
 Kadhalika alimalizia mazungumzo yake kwa kuashiria harakati za vikundi vya kigaidi akisema kuwa: watu na vijana wengi wamekuwa wanajiunga na vikundi vya kigaidi ikiwemo Daesh ni kutokana na msukumo wa sheria na maamuzi kama haya yasiozingatia haki za dini nyingine, hivyo tunapaswa kuzuia kusambaa kwa fikra za kigaidi kwa kusitisha utoaji wa sheria zinazo wanyima haki wafuasi wa dini zingine katika kutekeleza yanayopaswa katika imani zao.    
mwisho wa Habari/290